Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mashabiki wake,
wakishangilia baada ya Waziri huyo kutangazwa kuwa mshindi wa kura za
maoni ya kugombea ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakishangilia na wafuasi wao baada ya Nyalandu, kutangazwa kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini.
Na Mwandishi Wetu
………………………………..

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameibuka na ushindi wa kishindo katika
kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania ubunge Jimbo la
Singida Kaskazini.
kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania ubunge Jimbo la
Singida Kaskazini.
Nyalandu, ambaye alikitetea nafasi hiyo aliwashinda wagombea wenzake saba waliojitokeza
kupambana naye, ambapo aliongoza kwenye kata zote za jimbo hilo na kuwaacha
mbali wapinzani wake.
kupambana naye, ambapo aliongoza kwenye kata zote za jimbo hilo na kuwaacha
mbali wapinzani wake.
Mwanasiasa huyo kijana na mwenye ushawishi mkubwa, aliongoza katika Kata za Ikhanoda,
Msange, Itaja, Mwasauya, Mrama, Maghojoa, Ilongero, Ngimu na kuzidiwa kwa kura
chache kwenye kata moja ya Mughamo.
Msange, Itaja, Mwasauya, Mrama, Maghojoa, Ilongero, Ngimu na kuzidiwa kwa kura
chache kwenye kata moja ya Mughamo.
Matokeo ya mwisho yaliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi, yamempa ushindi Nyalandu kwa kupata
kura 13,738 huku akifutiwa na Justin Monko aliyepata kura 5,648.
kura 13,738 huku akifutiwa na Justin Monko aliyepata kura 5,648.
Nyalandu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, anamshukuru Mungu na wanachama wa CCM
jimboni humo kwa kumpa ushindi wa kishindo na wenye heshima licha ya kufanyiwa
mchezo mchafu na wapinzani wake.
jimboni humo kwa kumpa ushindi wa kishindo na wenye heshima licha ya kufanyiwa
mchezo mchafu na wapinzani wake.
Alisema wapinzani wake walicheza rafu za wazi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kuleta
makundi ya watu ambao hawakuwepo kwenye orodha ya wapiga kura, kuandaa vijana
wa kumzomea kwenye mikutano, lakini mwisho wa siku wananchi wameonyesha bado
wana muamini na kumchagua kwa kishindo.
makundi ya watu ambao hawakuwepo kwenye orodha ya wapiga kura, kuandaa vijana
wa kumzomea kwenye mikutano, lakini mwisho wa siku wananchi wameonyesha bado
wana muamini na kumchagua kwa kishindo.
“Nimekuwa kwenye siasa kwa muda sasa…lakini katika uchaguzi huu nimefanyiwa rafu nyingi
sana na wapinzani wangu ila nashukuru Mungu wananchi wameonyesha bado
wananiamini na imani hiyo inatokana na kazi kubwa niliyoifanya kama mbunge wao.
Nitaendelea kuwatumikia kwa juhudi na akili zangu zote na kamwe sitawaangusha,”
alisema Nyalandu.

No comments:
Post a Comment