Dkt
Regnald Mengi
Mwenyekiti
wa makampuni ya IPP Dkt Regnald Mengi ametangaza zawadi kwa vijana wote wa
kitanzania waliozaliwa mwaka 1994 wakati gazeti la Nipashe lilipoanza
kuchapishwa nchini.
Dkt
Regnald Mengi ambaye pia ni mwenyekiti wa makampuni ya IPP, ametangaza zawadi
hiyo jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika maadhimisho ya kusheherekea gazeti la
Nipashe kutimiza miaka 21 sokoni.
Kwa
uapnde wake mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Bw Jesse Kwayu amesema
kumekuwa na mafanikio makubwa tangu gazeti hilo linalotamba kwa habari za
uhakika lianzishe.
Aidha
ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa wataendelea kusimamia ukweli na kamwe
gazeti la Nipashe halitatumika katika kuunga mkono chama chochote cha kisiasa
hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Gazeti
la Nipashe lililokuwa kwenye muonekano mpya lilionekana kupendwa zaidi katika
siku yake ya kwanza kama ambavyo Bw John Magesa muuzaji wa magazeti
anavyozungumza.
No comments:
Post a Comment