Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi 
Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jioni hii katika ofisi 
ndogo ya Makao makuu CCM Lumumba wakati alipotangaza Kamati maalum ya 
Kampeni za uchaguzi mkuu ujao zinazotarajiawa kuzinduliwa Agosti 23 
mwaka huu.
Baadhi ya wapiga picha wa 
Televisheni na magazeti  kutoka vyombo mbalimbali wakipata picha wakati 
Katibu Mwenezi huyo alipokuwa akitangaza kamati hiyo.
……………………………………………………………………….
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake 
cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM 
Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta 
Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge 
katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.
Wagombea ubunge walioteuliwa 
kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu 
Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John 
(Kiteto).
Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi 
wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo 
itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa 
Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;
KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
- Ndugu Abdulrahman Kinana – Mwenyekiti
 - Ndugu Rajab Luhwavi – Makamu Mwenyekiti – Bara
 - Ndugu Vuai Ali Vuai – Makamu Mwenyekiti – Z’bar
 - Ndugu Sofia Simba
 - Ndugu Mohamed Seif Khatib
 - Ndugu Asha-Rose Migiro
 - Ndugu Samwel Sitta
 - Ndugu Nape Nnauye
 - Ndugu Mwigulu Nchemba
 - Ndugu Harrison Mwakyembe
 - Ndugu January Makamba
 - Ndugu Amina Makillagi
 - Ndugu Christopher Ole Sendeka
 - Ndugu Stephen Wasira
 - Ndugu Abdallah Bulembo
 - Ndugu Hadija Aboud
 - Ndugu Mohamed Aboud
 - Ndugu Lazaro Nyalandu
 - Ndugu Issa Haji Ussi
 - Ndugu Waride Bakari Jabu
 - Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
 - Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
 - Ndugu Maua Daftari
 - Ndugu Stephen Masele
 - Ndugu Pindi Chana
 - Ndugu Shaka Shaka
 - Ndugu Makongoro Nyerere
 - Ndugu Bernard Membe
 - Ndugu Sadifa Juma Khamis
 - Ndugu Antony Diallo
 - Ndugu Livingston Lusinde
 
32Ndugu Ummy Mwalimu 
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
No comments:
Post a Comment