ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALLA KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, August 26, 2015

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALLA KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM


????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula alipowasili katika eneo la Mtambo wa Ruvu juu Darajani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani Agosti 25, 2015  wakati wa ziara ya siku tatu ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo miradi hiyo inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA).
14
Ujenzi uifadhi wa pampu ukiendelea.
IMG_2598
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikagua moja ya transfoma ya umeme kwaajili ya kuongeza uwezo wa utendaji kazi wa mashine mpya zitakazo fungwa,Waziri  Amos Makalla anafanya ziara  siku tatu ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo miradi hiyo inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA).
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipata maelezo kutoka kwa Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi kuhusiana na upanuzi wa mtambo wa kuongeza uzalishaji kutoka mita za ujazo 82,000 hadi 196,000 kwa siku.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa ameongozana na wakandarasi wa miradi na maofisa kutoka Wizara ya maji. wakikagua ujazo wa maji ruvu Darajani.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla pamoja na wakandarasi wa miradi na maofisa kutoka Wizara ya maji. wakikagua wakiangalia kina cha maji kilipofikia.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Meneja mradi wa Kampuni ya WABAG kutoka India. Pintu Dutta (watatu kulia) Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula, Injinia Masudi Omari, Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi  wakikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha ruvu juu .
????????????????????????????????????
Wakiwa ndani ya Mtambo wa zamani wa kusukuma maji.
????????????????????????????????????
Ujenzi wa nyumba za wafakazi ukiendelea.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto), akiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula wakitafakali jambo kabla ya kuanza mazungumzo na wakandarasi wanaojenga mradi huo.
16
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla meza kuu mbele akifanya mazungumzo na maofisa wa Kampuni ya WABAG mara baada ya kufika katika eneo la upanuzi wa mtambo wakuongeza uzalishaji wa maji ulipo Mlandizi pamoja na kujionea ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na matanki ya machujio ya maji.
????????????????????????????????????
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa matanki ya maji.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada kukagua upanuzi wa mtambo wakuongeza uzalishaji wa maji ulipo Mlandizi pamoja na kujionea ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na matanki ya machujio ya maji.
????????????????????????????????????
Mafundi wa Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure  wakiendelea na ulazaji wa mabomba mapya ya maji eneo la Tumbi Kibaha.
????????????????????????????????????
Kutoka kulia ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati wa ziara ya siku tatu ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo miradi hiyo inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA).
????????????????????????????????????
Ujenzi wa tenki ruvu juu ukiendelea.
……………………………………………………
Picha zote na Alex John

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here