Msemaji wa Jukwaa la PoliDigita Arbogast Matokeo akizungumza na waandishi wa habari anayefatia ni Emanuel Ernest ambaye ni operation
and logistics Officer.
WATAALAMU wa mifumo ya taarifa za Kijiografia (GIS), wameanzisha Jukwaa linalowaleta pamoja wanasiasa, vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla ili kurahisisha shughuli za kampeni kufanyika kidigitali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu.
Aidha jukwaa hilo linalojulikana kwa jina PoliDigita litaanza kufanya kazi pindi wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu watakapoanza kampeni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jukwaa hilo, Arbogast Matokeo, alisema lengo la kuanzisha jukwaa hilo ni kukutanisha vyama vya siasa na wapiga kura wao ili waweze kunadi sera zao kwa njia ya mtandano.
Alisema wananchi watapata fursa za kuzijua sera za wagombe wa nafasi mbalimbali pamoja na kushindanisha sera zao ili waweze kupata kiongozi bora na anayeweza kuwatatulia shida zao ndani ya jamii.
“Ndani ya jukwaa hilo kutakuwa na wanachama ambao ni vyama vya siasa, wagombea na wananchi ambao ndio wapiga kura wao, hivyo kutakuwa na sehemu za kuweka wafisu wa mgombea pamoja na kunadi sera zake,” alisema.
Aliongeza kuwa wagombea wa nafasi ya Urais na Ubunge watasajiliwa bure, huku vyama vya siasa vikitakiwa kuweka wasifu wao na wananchi kupata uhuru wa kuchagia na kupigia kura sera zao.
Alisisitiza kuwa kwa wananchi ambao wapo mikoani na vijijini wataweza kushiriki katika jukwaa hilo kwa kutumia simu za mikononi ambapo watapokea kila taarifa mpya na sera zitakazowekwa na wagombea wao.
Kwa upande wa Meneja uendeshaji wa jukwaa hilo, Emanuel Ernesty alisema katika shughuli za uendeshaji wa jukwaa hilo wamezingatia maadili ya mitandao ili kuwalinda watumiaji.
Alisema wameweka mifumo ya kudhibiti uharibifu aua wizi wa taarifa za wagombea ili kuhakikisha watumiaji waendesha shughuli zao bila kuchafuana wala kutoleana maneno machafu.
“Katika jukwaa hili hatutoruhusu siasa za kuchafuana au wananchi kuwatolea maneno ya machafu wagombea kama zile zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii sisi tumeweka utaratibu wa kuwalinda wanachama wote,”alisema.
No comments:
Post a Comment