Hali ilivyokuwa katika barabara ya Bibi Titi na Morogoro.
Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa wakiwa kwenye gari kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kumsindikiza Mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa.
…umati uliofurika.
Wafuasi wa vyama vyote wakiwa juu ya gari lao kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumsindikiza Lowassa.
Gari
la Mhe. Lowassa likisindikizwa kuelekea Makao makuu ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kinondoni mara baada ya kuchukua fomu.
Wananchi barabarani wakimlaki Lowassa kwa kuonesha ishara ya Chadema.
Ulinzi ulivyoimarishwa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe
alipowasili katika ofisi za Chama Cha wananchi (CUF) asubuhi ya leo
kabla ya msafara kuanza.
James Lembeli akisalimiana na mmoja wa viongozi wanaounda Ukawa.
Kamanda mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga akibadilisha neno na askari mwenzake kama inavyoonekana pichani.
Ester Bulaya (aliyeko juu ya gari kulia akiwa kwenye msafara huo.
Taswira ya msafara wa Lowasa.
Hatimaye
mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Waziri Mkuu
mstaafu Edward Ngoyai Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea nafasi
hiyo katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Awali,
mgombea huyo alianzia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF),
Buguruni, Dar es Salaam kisha kuelekea Tume yaTaifa ya Uchaguzi kwa
kupitia barabara ya Uhuru, Bibibti Mohamed hadi Makao Makuu ya Tume
hiyo.
Baada
ya hapo, msafara wake ulipititia Barabara ya Ocean Road kisha Umoja
wa Mataifa, Ally Hassan Mwinyi hadi Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Katika msafara huo, umati mkubwa wa wapenzi na wakereketwa wa mgombea huyo walijitokeza kumsindikiza .
Wananchi wamejitokeza kwa
wingi leo kumsindikiza Edward Lowasa kwenda kuchukua fomu ya kugombea
nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha
Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA).
Msafara ulianza rasmi kutoka katika ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC Taifa.
![]() |


![]() |
Jiji la Dar es salaam leo ilikuwa kama ni sikukuu hivi baada ya LOWASA kufunga kazi za watu na kuambatana nao kwenda kuchukua form ya Urais,hapa kuna picha ambazo tumezinasa katika tukio hilo zikionyesha matukio ambayo yamesisimua sana katika matembezi hayo yaliyozunguka sehemu kubwa ya jiji la Dar es salaam leo hii,Huyu ni mbunge Tundu Lissu akiwa ameshikilia kadi yake ya mpiga kura akiwaonyesha wanachama waliojitokeza leo |
![]() |
Bodaboda |
![]() | |
Yero |
![]() |
Katika hali ya kushangaza gari la maabusu lilipita maeneo yale wakati likienda mahakamani na ikawabidi kusimama na kuanza kushangilia kwa ishara ya vidole viwili yani CHADEMA |









afe kipa afe beki lowasa ndio raisi hahahahaha.......!
ReplyDelete