Tangu
chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA kibadilishe njia yake ya
kuusaka uongozi wa Taifa hili kwa kumsajili waziri mkuu mstaafu Edward
lowasa kumekuwa na story mfululizo zilizokuwa zinaeleza kuwa kuna baadhi
ya viongozi wa chama hicho wamesusa kushiriki katika vikao vya chama
hicho kutokana na kutokubaliana na uteuzi wa mh LOWASA.
Viongozi
waliokuwa wanatajwa ni pamoja na mwasheria wa chama hicho Mh TUNDU
LISSU,na Naibu katibu mkuu Bara mh JOHN MNYIKA ambao kwa pamoja
walihusishwa katika sakata hilo.
Leo inaweza kuwa ni mwisho wa
story hizo baada ya viongozi hao kuonekana katika mkutano mkuu wa baraza
kuu la chama hicho KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA tofauti na wengi
walivyodhani kuwa hawatashiriki katika vikao tena.
Mh mnyika
akizngumza na mwandishi wa mtanzao huu amesema kuwa sababu pekee
iliyomfanya asionekane kwa kipindi kirefu tokea usajili wa LOWASA
ufanyika ni matatizo ya kiafya na sasa yupo fiti kukitumikia chama
hicho. |
No comments:
Post a Comment