Mtia
nia ya urais kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Aliyejiuzulu, Edward Lowassa
akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kimteue kugombea nafasi hiyo
kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Prof. Abdalaah Safari
(kushoto) kwenye
Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Katibu
Mkuu wa
CHADEM. Lowassa alikuwa ni kada wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi na
alijiunga na Chadema hivi karibuni baada ya kuenguliwa na CCM katika
mbio za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea Urais.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Prof. Abdalaah Safari (kushoto) akipeana mkono wa shukrani na Mtia nia ya urais kwa Chadema, Edward Lowassa baada ya kupokea fomu zake.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Prof. Abdalaah Safari akifurahia jambo na Edward Lowassa wakati akipitia fomu hizo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na mmoja wa wanasheria mashuhuri Mabere Marando akipitia fomu hizo
Mabere Marando akifdurahia jambo na Edward Lowassa baada ya kupokea na kuzipitia fomu zake.
Wanachama wa Chadema ambao ni wabunge wa Chama hicho wakifuatilia tukio hilo.
Lowassa akiondoka baada ya kurejesha fomu.
No comments:
Post a Comment