
SIKU
Chache kupita baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kutangaza kujiuzulu
nafasi ya uwenyekiti ndani ya Chama cha wananchi CUF, Hatimaye Chama
hicho kimeunda kamati ya mda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia
nafasi za uongozi .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Hatua
hiyo imetangazwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya
kumalizika Kikao cha Dharura cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama
hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba.
Ambapo Seif amesema katokana na Kanuni za CUF wamefikia kwa
pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi
sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya uenyekiti.
Amesema Kamati hiyo
itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti
wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima na Kamati hiyo
itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama
vyengine vinavyounda UKAWA ambapo anadai itakuwa na jukumu lingine la
kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.
No comments:
Post a Comment