Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya
Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu
ya Chama
hicho,Lumumba jijini Dar,kuhusiana na madai ya kauli inayodaiwa kutolewa
na Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli kuwa kupitia Ilani
yake ya chama atatoa kompyuta kwa Walimu nchi nzima iwapo CCM itapita
madarakani,habari ambazo Nape amezikunusha vikali na kusema hayo ni
maneno ya uzusihi na kuwa Dkt Magufuli hajawahi kutamka maneno hayo
popote pale.
Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana
Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na
inatarajiwa kuzinduliwa Agosti
23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.Nape amefafanua kuwa kauli yoyote iliyotoka kwa
chama
hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani ya chama cha CCM,siyo ya
kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti
23" alisema na Nape kwa msisitizo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar. (Picha na JIACHIE BLOG)
NA BAKARI ISSA WA GLOBU YA JAMII.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali
kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe
Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.
Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.
Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.
Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.

No comments:
Post a Comment