Mtia nia ya ubunge kwa CCM Philemon Mollel
akizungumza katika mkutano wa kujinadi mbele ya wana CCM wa kata ya
Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake
kuwania ubunge wa jimbo la Arusha katika uchaguzi wa mwezi Oktoba Mwaka
huu.
(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia
nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake
mbele ya wanachama wa chama hicho katika kata ya Sakina jijini Arusha
ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwamgombea wa ubunge jimbo la Arusha
kupitia CCM.
Mtia nia ya ubunge kupitia CCM mwanasheria Victor Njau
akimwaga sera zake mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili
kuomba ridhaa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa mwezi
Oktoba mwaka huu.
Wanachama na waasisi wa CCM wa kata ya Sakina jijini Arusha
wakisikiliza kwa umakini sera zinazotolewana watia nia ya ubunge wa
jimbo la Arusha walipokua wakijinadi kwao ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa
na chaa chao kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Rais,Wabunge
na Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kada wa CCM Mosses Mwizarubi anayeomba ridhaa yakuteuliwa
na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha akisisitiza jambo
katika mkutano wa kujinadi uliofanyika katika kata ya Ngarenaro jijini
Arusha.
Mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM Hamis
Migire akijieleza mbele ya wanachama wa CCM wa kata ya Sokon One jijini
Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti hicho kupitia
CCM.
Mmoja wa wanachama wa CCM wa kata ya Sakija jijini Arusha
ambaye hakujulikana jina lake mara moja akipitia kwa umakini kipeperushi
chenye maelezo binafsi na mikakati ya kazi za ubunge cha mtia nia ya
ubunge wa chama hicho Mustafa Panju wakati wa mkutano wa kujinadi wa
watia nia hao uliofanyika katika kata hiyo.
Team kanitangaze wakifuatilia hotuba za watia nia ya ubunge kupitia CCM katika kata ya Elerai jijiniArusha
Hapa ni sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba mbalimbali za watiania nafasi ya Ubunge
Wananchi waliojitokeza kuwasikiliza watia nia Ubunge CCM katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha
No comments:
Post a Comment