Askari wakiwa pembezoni mwa Bunduki 14 na risasi 28 zilizokamatwa hivi karibuni, silaha hizo ni miongoni mwa silaha zilizoibwa juzi katika kituo cha polisi cha Staki shari kilichopo ukonga jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiwaonyesha waandishi wa habari na wananchi baadhi ya silaha zilizokamatwa kutokana na msako mkali unaoendelea jijini humo,Silaha hizo ziliibiwa katika kituo cha polisi cha Staki shari kilichopo ukonga.
Akionesha silaha zilizokamatwa kwa waandishi wa habari na wananchi waliofika kwenye tukio hilo.
fedha zilizokamatwa milioni 170.
Akionesha fedha zilizokamatwa Sh milioni 170.
Pesa walizokutwa nazo watuhumiwa zikiwa zimehifadhiwa kwenye sanduku la chuma.
Kamishna Kova akionyesha picha za watuhumiwa wanaotafutwa na jeshi la polisi.
Pikipiki zilizotumika kwenye ujambazi wa wizi wa silaha za kituo cha polisi cha Stakishari, Ukonga na zoezi la juzi lililotaka kufanyika.
Kamanda wa Operesheni wa Kanda hiyo, Simon Sillo naye alipata nafasi ya kuzungumza katika mkutano hu. (Picha zote na Elisa Shunda).
Kamishna Kova alisema bunduki 14 na risasi 28
ambazo ziliibwa na majambazi kwenye
kituo hicho cha SitakiShari zimekamatwa zikiwa
zimefukiwa ardhini katika kijiji cha Mandimkongo kilichoko wilayani Mkuranga
mkoa wa Pwani.
Bunduki hizo 14 ni kati
ya silaha 16 zilizokamatwa na polisi wakati wakiwa kwenye upelelezi wa tukio
hilo ambalo liliacha polisi wanne na raia watu wakiuwa na majambazihao.
Licha ya bunduki hizo,
polisi pia wamekamata risasi 53, fedha taslimu Sh Milioni 170 pamoja na watu
watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baadhi yao wakiwe waliohusika na tukio
la Stakishari.
Miongoni mwa silaha hizo
14 ambazo zimetambulika kuwa ziliibiwa
hivi karibuni katika kituo cha Stakishari Julai 12 mwaka huu, zimo bunduki aina
SMG 7, SAR 7 na Risasi 28 zilizoporwa katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment