MABORESHO: TANESCO YAJA NA NGUZO ZA ZEGE KUKABILIANA NA UCHAKAVU WA MARA KWA MARA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, July 22, 2015

MABORESHO: TANESCO YAJA NA NGUZO ZA ZEGE KUKABILIANA NA UCHAKAVU WA MARA KWA MARA

 
 Hizi ndio nguzo mbazo hazitatuika tena na tanesco kiwanda kitatapokamilika.


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lipo katika mchakato wa mwisho wa kuanzisha Kampuni ya kutengeneza  nguzo za umeme za zege, ili kuongeza ubora sambamba na kukidhi mahitaji ya nguzo huku hiyo ikiwa ni mkikakati ya uboreshaji huduma kwa wateja wake.

 Mkurugenzi wa  (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba, anasema kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya Shirika hilo inatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu, mchakato wa kuisajili kwa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (Brela) utakapo kamilika.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Felchesmi Mramba.

 
Alisema hatua ya shirika hilo kuanza kutumia nguzo za zege badala ya zile za mbao, ni moja ya mikakati ya Shirika ilo kuhakikisha linatoa huduma bora na ya uhakika kwa wateja wake kwani mara nyingi nguzo za mbao zimekuwa hazidumu na kulazimisha kubadilishwa mara kwa mara kutokana na uchakavu wake.

“Teknolojia inakuwa kila siku na kurahisisha huduma kwa wananchi na hata wakati mwengine kupunguza gharama, tutakapoanza kuzalisha nguzo za zege tutapunguza kero nyingi kwa wateja wetu kwani nguzo za mbao kuaribika hasa kipindi cha mvua pamoja na moto kuunguza nguzo sehemu za misitu ambazo nguzo zetu zimepita,”alisema Mramba.

Anasema kuwepo kwa nguzo hizo za zege kutabadilisha madhali ya jiji na kuongeza mvuto sambamba na kuwa imara, na pindi Kampuni hiyo itakapoanza kazi itasaidia  kwa kiasi kikubwa kuongeza fursa kwa watanzania kwa kupata ajira.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here