Katibuu
Mwenezi wa CCM Kata ya Msasani, Bw. Andrew Mangole (kulia) akiwaomba
wana CCM kuachana na makundi na baadala yake wakijenge chama katika
misingi imara na kuibuka na ushindi hapo baadae katika uchaguzi Mkuu.
(Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Magomeni-Kinondoni)
Kampeni za kura za maoni kwa wagombea Udiwani ndani ya Cha Cha
Mapinduzi (CCM) zimepamba moto ambapo kila mgombea amejitokeza na
kujinadi mbele ya wanachama ili achaguliwe kukiwakilisha chama hicho
katika uchaguzi mkuu hiyo Oktoba mwaka huu.
Kata
ya Magomeni kwa nafasi ya Udiwani ndani ya CCM inawaniwa na Makada wane
akiwemo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni ambaye anatetea kiti
chake, Dk. Julian Bujugo. Wengine wanaowania katika uchaguzi huo ni
pamoja na Nurdin Butembo, Gardiner Dibibi na Sadique Bwanga.
Awali
wagombea hao walianza upande wa Magomeni Makuti ndani ya Kata hiyo ya
Magomeni kwa kujinadi kwa Wanachama wa CCM na kisha kuhamia upande wa
Magomeni Mapipa ndani ya Ofisi za CCM Kata.
Kwa
upande wake mgeni mwalikwa ambaye ni Katibuu Mwenezi wa CCM Kata ya
Msasani, Bw. Andrew Mangole aliwaomba wagombea wote wanne kuzingatia
maadili ya chama na wagombea kujinadi bila kukashifiana ilikukijenga
chama
“Tufanye
kampeni kistaarabu. Wagombea wote wazuri na munasifa ndani ya chama ila
hapo Agosti Mosi kura zitakazopigwa anatakiwa mmoja tu ashinde na
wengine mutakuwa bora zaidi ila kura hazitowatosha ila kwa watakao kuwa
kura hazijatosha muendelee kuungana na chama kuleta ushindi wa kishindo”
alieleza Katibu Mwenezi huyo Mangole.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kata Magomeni, Shaweji aliimiza umoja
na ushirikiano kwa wana CCM wote kuakikisha wanaleta ushindi ndani ya
chama na nje ya Chama kwa Kata hiyo kuwa chini ya CCM kuendeleza
maendeleo ya Kata hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Magomeni CCM, Sadique Kudulo alieleza kuwa
CCM ni chama tawala hivyo kitaendelea kuongoza dola kwa misingi
thabiti huku akiwataka wana CCM kutofanya makosa kwa kuchagua mgombea
atakaye kiuza chama na kisha kuibuka kidedea katika uchagui hapo baadae.
Aidha,
wagombea wote wameweza kujielezea kwa wana CCM kwa kujinadi na kisha
kuomba kupigiwa kura hiyo tarehe 1.8.2015. ambapo katika uchaguzi huo wa
ndani anatakiwa mgombea mmoja tu apaatikane na kisha jina lake
kupelekwa ngazi ya juu ya chama na kisha kurejeshwa baada ya kujadiliwa
kwa kina ili kusimamishwa kugombea katika uchaguzi hiyo Oktoba.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Magomeni, Shaweji akisisitiza jambo katika mkutano huo wa kampeni za udiwani ndani ya CCM
Katibuu Mwenezi wa CCM Kata ya Msasani, Bw. Andrew Mangole akitoa akitoa nasaha zake kwa wana CCM (Hawapo pichani).
Aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Magomeni ambaye anatetea kiti chake katika Kata hiyo,
Dk. Julian Bujugo akijinadi kwa wana CCM leo Julai 28.2015 Katika
ofisi za CCM Kata.
PICHA
ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya
Chama hicho, Kijana Sadique Bwanga akiomba kura kwa wana CCM
waliojitokeza katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai
28.2015 katika ofisi za CCM Kata.
PICHA
ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya
Chama hicho, Kijana Gardner Dibibi akiomba kura kwa wana CCM
waliojitokeza katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai
28.2015 katika ofisi za CCM Kata.
…naomba kura yenu.
PICHA
ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya
Chama hicho, Bw. Nurdin Butembo akiomba kura kwa wana CCM waliojitokeza
katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai 28.2015 katika
ofisi za CCM Kata.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Sadique akitoa sisitiza wana CCM kuwa kitu
kimoja pamojana kuepuka kampeni za matusi ilikukijenga chama .. wakati
wa tukio hilo la kampeni za ndani..
No comments:
Post a Comment