RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi
amewataka watendaji wa halmashauri nchini kuendeleza mshikamano na ushirikiano
katika dhamira moja ya kuwatumikia wananchi ili waweze kupiga hatua katika
maendeleo.
Mwinyi
aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuvunja Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kusisitiza kwamba sehemu
yenye mshikamano ndiyo yenye maendeleo.
Akizungumzia
masuala ya kisiasa alisema kuwa, “nchi yetu sasa ipo katika shughuli za kisiasa
za kutafuta viongozi bora, lakini Yule mwenye maarifa ni mwenye uzoefu wa
kufikia maendeleo.”
Mapema
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty alisema kwa kipindi cha miaka
mitano wameshirikiana mengi na madiwani hao na kufanikiwa kupiga hatua
mbalimbali ambapo kwa mwaka 2009/2010 walikuwa wakikusanya Sh bilioni 11.6
lakini kwa sasa wanakusanya Sh bilioni 38.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda alisema wamefanya mambo mengi
kwa ushirikiano katika sekta ya elimu, afya na maji ambapo pia wanatarajia kutengeneza
ajira zaidi ya 1000 katika kiwanda cha kuchakata taka.
No comments:
Post a Comment