
Mungoza
watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini
Zimbabwe, Aleck Makumire akitoa maelezo wa timu ya waandishi wa habari
kabla ya kushuka kwenye mapango hayo wakati wa ziara maalum ya
kutembelea vivutio vya Utalii nchini humo.
*************
Na Modewjiblog team, Harare
Waandishi
wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo
mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African),
Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog),
Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa
Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe
(ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la
ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja
na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Safari
ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga
wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya
kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare.
Safari
hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa
ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza
kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference
Centre (HICC).

Mungoza
watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini
Zimbabwe, Aleck Makumire akiwa ndani ya mapango ya Chinhoyi akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari wa Tanzania katika ziara yao ya
kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.
Waandishi
wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye
gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii
ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy
Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na
Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi
huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
Mwandishi
wa habari Timothy Kitundu (East Africa Business Week) akitoka kudhuru
mapango hayo wakati wa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.



No comments:
Post a Comment