BILIONEA wa Nigeria Aliko Dangote amepanga kuinunua
klabu ya Arsenal. Bilionea huyo anaamini jinsi alivyowekeza kwenye mafuta na
majengo nchini mwake anaweza kuwa na fedha za kuinunua klabu hiyo ya England.
Dangote
mwenye umri wa miaka 58 ambaye inakadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani
bilioni 11.5 alisema amekuwa akiishabikia the Gunners tangu miaka ya 1980.
"Nitakapopata
nafasi hiyo nitakuwa na vyanzo vya kutosha kuinunua,” alisema alipoulizwa na
BBC.
Mmarekani
Stan Kroenke ni miongoni mwa mwanahisa wa Arsenal akimiliki asilimia 66.64.
Mrusi
Alisher Usmanov anamiliki asilimia 29.11 na nyingine 62,217 zikimilikiwa na watu mbalimbali wakiwemo
wachezaji wa zamani na mashabiki wa Arsenal. Dangote anashika nafasi ya 67
katika orodha ya matajiri duniani.
Siku
za nyuma alikuwa akitaka kununua asilimia 15.9 ya hisa kwa Kroenke kwa dola za
Marekani milioni 123.
"Tulikuwa
wengi tuliotaka kununua hisa, lakini watu waliokuwa wakifanya biashara
walitangaza dau la kutuua,” aliongeza Dangote.
Dangote
anaamini Arsenal inatakiwa kumilikiwa na watu tofauti tofauti ili ipate
mafanikio makubwa uwanjani.
Aliongeza:
"Wanafanya vizuri, lakini wanahitaji mkakati mwingine zaidi, wanahitaji
mkakati wa kimwongozo kuliko ilivyo sasa ambapo wanaendeleza vipaji na kuuza”.
No comments:
Post a Comment