Friday, June 5, 2015

YAMOTO KUZINDUA MADOIDO ESCAPE ONE KESHO

 
BENDI ya Yamoto bendi itafanya uzinduzi wa wimbo wake mpya wa Cheza Kimadoido siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Escape One Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jiji Mkurugenzi wa bendi ya Yamoto, yenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam, Said Fella ‘Mkubwa na Wanawe’, aliwaomba Watanzania kuwaunga mkono vijana wao kwa kujumuika nao siku hiyo.

“Tunashukuru kwa kuipokea ngoma hii kwa mikono miwili na tunaomba muendelee kuwasapoti katika muziki wao  ili uendelee kukua,” alisema Fella.

Kwa mujibu wa Mkubwa Fella, wasanii ambao watasindikiza uzinduzi huo ni bendi ya Mapacha Watatu, Tunda Man, Madee, Chege na Temba.

Bendi ya Yamoto ambayo inafanya vizuri katika soko la muziki huo, inaundwa na wasanii wanne ambao ni Aslay, Maromboso, Beka One na Enock Bella.

No comments:

Post a Comment