BENDI ya Yamoto bendi itafanya uzinduzi wa wimbo
wake mpya wa Cheza Kimadoido siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Escape One
Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jiji Mkurugenzi wa bendi ya Yamoto, yenye maskani yake
Temeke jijini Dar es Salaam, Said Fella ‘Mkubwa na Wanawe’, aliwaomba
Watanzania kuwaunga mkono vijana wao kwa kujumuika nao siku hiyo.
“Tunashukuru kwa kuipokea ngoma hii kwa mikono miwili na tunaomba
muendelee kuwasapoti katika muziki wao
ili uendelee kukua,” alisema Fella.
Kwa mujibu wa Mkubwa Fella, wasanii ambao watasindikiza uzinduzi huo ni
bendi ya Mapacha Watatu, Tunda Man, Madee, Chege na Temba.
Bendi ya Yamoto ambayo inafanya vizuri katika soko la muziki huo,
inaundwa na wasanii wanne ambao ni Aslay, Maromboso, Beka One na Enock Bella.
No comments:
Post a Comment