Saturday, June 6, 2015

WANAOKWEPA USHAHIDI WANACHANGIA MAUJAI YA ALBINO

TABIA ya watu kukwepa kutoa ushahidi mahakamani, imetajwa kuwa sababu mojawapo inayochangia kukosekana kwa ushahidi dhidi ya wahalifu wa mauaji ya albino. 

Hayo yalielezwa katika warsha zilizoendeshwa mfululizo wilayani Misungwi, Kahama na Bariadi za ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia na kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Wakichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi, washiriki wamesema imekuwa kawaida kwa watu kutokuwa tayari kutoa ushahidi mara wanapoitwa mahakamani, kwa sababu zisizokuwa na mashiko.

Sababu hizo ni kuogopa kuuawa na wahusika na shinikizo kutoka kwa wanafamilia.





No comments:

Post a Comment