VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kutojihusisha na
kampeni chafu za siasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu
ndani ya nyumba za ibada.
Aidha
wametakiwa kutotoa fursa kwa baadhi ya wanasiasa watakaotaka kutumia nyumba
hizo za ibada kufanya kampeni zao, kwa kuwa nyumba hizo takatifu zipo kwa ajili
ya Mwenyezi Mungu.
Akizungumza
wakati wa kufungua semina kuhusu majukumu ya kijamii na kisiasa kwa walimu wa
madrasa wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema, hata kama ni
kiongozi wa dini ana chama chake anachokipenda hana nafasi ya kukipigia kampeni
katika nyumba za ibada kwani kwa kufanya hivyo italeta mkanganyiko kwa waumini.
“Kama
kiongozi wa dini una chama chako, kuna mahala sahihi kwenye majukwaa, lakini si
kwenye nyumba za ibada. Kila muumini ana chama chake sasa wewe utakapopiga
kampeni ya chama chako unaweza ukakuta waumini wanakimbia au kila mmoja anakuja
na sare ya chama chake, hivi itakuwaje?” alihoji Sadiki.
Kwa
upande wake, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu Wasomeshao Quran nchini (JUWAQUTA), alisema,
lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha walimu hao wajibu wao katika masuala ya
kijamii, kisiasa na kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
mkuu.
Alisema
walimu hao ni wadau wakubwa katika masuala ya usalama, upendo, mshikamano wa
dini na dini, hivyo serikali iwatazame walimu hao kuwa ni watu wanaohitaji
kushirikishwa katika mambo mbalimbali nchini.
Aidha,
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani, Stefan
Reith alisema, wanafanya kazi kwa karibu na Juwaquta hasa katika kuhamasisha
masuala ya amani
No comments:
Post a Comment