SERIKALI imetuma Sh bilioni 10 katika mikoa mbalimbali
nchini kwa ajili ya kuwalipa walimu wapya ambao wameripoti kazini mapema mwezi
uliopita.
Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo bungeni wakati alipotoa ufafanuzi
kwa Mwongozo kwa Spika ulioombwa na Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
(CCM).
Rage
katika Mwongozo wake , alitaka kusikia kauli ya Serikali kuhusu walimu wapya
ambao wamepangwa katika Manispaa ya Tabora na sehemu nyingine nchini kuwa
hawajapewa fedha zao na wanaishi katika hali ngumu kwa sasa.
Naibu
Waziri alikiri kuwa ni kweli wapo walimu katika baadhi ya halmashauri nchini,
hawajalipwa fedha zao baada ya kuripoti kazini kutokana na sababu mbalimbali.
"Ni
kweli wapo walimu hawajalipwa fedha zao kama alivyoeleza Mheshimiwa Rage. Yapo
maeneo kadhaa nchini na hii imetokana na matatizo kati ya wizara husika na
hazina," alisema Mwigulu na
kuongeza:
"Ni
kama nilivyoeleza hapa juzi kuwa watumishi wanapopangwa ni lazima kila kitu
kikamilishwe, sasa hapa kulikuwa na tatizo katika maandalizi yao.
"Lakini
jana (juzi) watu wa Hazina wamenihakikishia kuwa shilingi bilioni kumi
zimeshapelekwa huko na sasa ni suala tu la kufikishwa kwa wahusika."
Serikali
ilitangaza kuanza kwa ajira za walimu wapya Mei Mosi mwaka huu.
Idadi
ya walimu wapya walioanza ajira hizo ni 31,056 ambapo kwa walimu wa ngazi ya
Cheti ni 11,795, Stashahada 6,596 na
wenye Shahada 12,665.
No comments:
Post a Comment