TSN Group Tanzania,
katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, imeingia
mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum
kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo.
“Tunarahisisha na
kuboresha huduma zetu kuwa bora na za kisasa. Pengine huduma hii itapanua wigo
wa wateja wetu watumiao Black Cards kwa Dar es salaam lakini kwa Mwanza TSN
Hypermarket inakuwa kampuni ya kwanza kupokea na kukubali malipo kupitia Black
card ya Mimosa. Hatua ambayo ni kubwa kuchukuliwa na TSN katika kuwajali wateja
wake.”
“Sasa ukifanya
malipo kupitia kadi ya Mimosa kwenye supermarket zetu na Petrol station
unajiweka katika nafasi ya kushinda punguzo la zaidi ya asilimia 5 pamoja na
kuponi ya zawadi wa kwateja watakao tumia kiasi cha shillingi laki moja kwa
manunuzi ya mara moja,” alisema Jahu.
Akieleza zaidi juu
ya huduma na faida wazipatazo wateja watumiayo kadi hizo, Mkurugenzi Msiaidizi
wa MIMOSA, Leonce Mongi alisema kupitia kadi hii Mteja wa TSN hatapata tu punguzo
la bei kutoka TSN pekee lakini pia atapata offer mbalimbali zitokanazo na kadi
hiyo kupitia discount partners wengine ambao ni zaidi ya watoa huduma 71 Nchi
Nzima.
Jahu alisema TSN inajiimarisha katika kutoa huduma zake kwa wateja,
kuwasikiliza na kuwasaidia, hivyo basi kuona umuhimu wa kuwapatia wateja wake
wenye MIMISA black card nafasi ya kufanya malipo yao kwa uhuru na furaha.
Alisema,”hatua hii
inafuatia hatua nyinginezo nyingi tulizochukua kuhakikisha wateja wa TSN
wanafurahia huduma zetu, ikiwemo malipo kutupitia miamala ya simu, bank
cheques, malipo ya dola na sasa pia kupitia Mimosa Black Card.
Leonce alisema
kupitia kadi hii TSN itakuwa ikipokea malipo na kuongezaa tija kwa mteja, lengo
ni kuhakikisha mteja mwenye kadi ya Mimosa hashindwi kufanya malipo yake
akiwepo katika vionga vyao, na pia kufurahia ofa na punguzo mbalimbali zipatikanazo
na mtangamano huu.
“Teknolojia
imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na kuongeza
ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika nyanja mbalimbali za
kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta matokeo chanya siku hadi siku.
Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji kazi lakini pia upokeaji wa huduma
mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa kawaida kumerahisishwa.” Alisema Jahu.
Katika kutambua fursa hiyo, TSN itaendelea
kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi zinaenda sambamba na
mabadiliko hayo ya teknolojia.
Leonce aliipongeza TSN kwa kuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha inaweka urahisi kwa wateja wake na hiyo imekuwa ni
chachu kubwa katika kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.
No comments:
Post a Comment