UNGA WA MAHINDI WAMNUSURU NA KIFO - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, April 19, 2017

UNGA WA MAHINDI WAMNUSURU NA KIFO

Image result for ziwa malawi 
Mzee Granciam Kondowe amenusurika kufa maji kwa kushikilia mfuko wa unga wa mahindi baada ya mashua aliyokuwa akisafiria kuzama katika Ziwa Malawi.

Kondowe (67) ni miongoni mwa abiria 54 ambao polisi wamesema wal;inusurika baada ya boti kupinduka kutokana na hali mbaya hewa siku ya Jumapili.

Kwa mujibu wa Polisi nchini humo, watu watano walikufa maji huku 111 wakiwa hawajulikani waliko .

Mashua hiyo ilikuwa imewabeba waumini waliokuwa wakirejea kutoka katika sherehe za Pasaka ilipopinduka katika wilaya ya Rumphi, kaskazini mwa Malawi.

Kondowe alieleza kituo cha kibinafsi cha radio, Zodiac, kuwa upepo mkali ulivuma kwa dakika 15 baada yao kuanza safari.

Wafanyakazi waliamua kuirejesha mashua ufuoni lakini boti lilizama kabla hawajafika, alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here