SARATANI YA DAMU (LEUKEMIA) Leukemia ni Saratani
inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph
(lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya
damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na
nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.
Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white
blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye
maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya
chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi
mbalimbali.
Leukemia husababishwa na nini
Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha
leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia
hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu
sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya
DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya
kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa,
vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na
sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA
hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na
tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa
kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi
inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye
kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.
kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.
Je, kuna vihatarishi vya leukemia
Ndiyo vipo! Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu
hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata
ugonjwa wa saratani ya damu.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:
Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla: Watu ambao wamekuwa kuwa na
aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa
tiba ya mionzi au madawa makali ya
saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa sababu
baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli
nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki sawasawa
uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba kama vile
ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika
kuugua pia ugonjwa wa saratani ya damu.
Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa mengine ya damu
kama vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa na
kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa
yaanimyelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua
saratani ya damu.
Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi kupigwa na
kiasi kikubwa cha mionzi kama vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa
vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya
kupata saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza
Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza
magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu.
Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao, baadhi ya
ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa wa
kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia
inaambukizwa isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha
ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi kukumbana
na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia, kadhalika
wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja kati
ya hivi.
MATIBABU YA SARATANI YA DAMU
Matibabu hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa ilipofikia.
Kwanza safisha damu yako
Zipo dawa nyingi za asili ambazo hutibu kansa , dozi ni kulingana na aina ya kansa na stage ilipofikia
Mfano Majani ya mstafeli yana uwezo wa kuziua seli za kansa aina yeyote mara 10,000 ya mionzi.
Chukua majani ya mstafeli yaaafishe vizuri kisha yaponde kwa Blenda kutengeza juisi yake
Mgonjwa anywe nusu kikombe kutwa mara tatu siku 90
Kwanza safisha damu yako
Zipo dawa nyingi za asili ambazo hutibu kansa , dozi ni kulingana na aina ya kansa na stage ilipofikia
Mfano Majani ya mstafeli yana uwezo wa kuziua seli za kansa aina yeyote mara 10,000 ya mionzi.
Chukua majani ya mstafeli yaaafishe vizuri kisha yaponde kwa Blenda kutengeza juisi yake
Mgonjwa anywe nusu kikombe kutwa mara tatu siku 90
SOURCE: MZIZI MKAVU BLOG
No comments:
Post a Comment