"Hii
achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone",
Mzee aliyejitaja kwa jina la Mandela, alimtambia Makonda huku akipiga
funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu
kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa mkoa.
Baadaye
alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa
kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi
kwa wasichana wenye umri mdogo.
Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga Makonda, ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika hodi yake.
"
Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote.
sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu" Kijana mmoja mwenyeji wa
eneo hilo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shuleya Msingi Tandale Makonda
alisema, serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo
hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili
vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi. badala ya kuliacha eneo
hilo liharibu maisha ya vijana.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akibisha hodi kwenye mlango
mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika
eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya
Manzese, akiwa katika siku ya tisa ya ziara yake mkoani humo leo. Kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi. Ebdelea kuona taswira
mbalimbali katika picha kama zilivyopigwa na Blogger na Msimamizi Mkuu
wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ameambatana na Makonda kwenye
ziara hiyo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, akimsaidia Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kubisha hodi kwenye mlango mmoja
katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo
maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhiwa bia na mhudumo wa
baa pekee aliyoikuta ikiwa wazi, wakati wa ziara hiyo katika eneo la
Uwanja wa Fisi
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiichunguza kwa makini bia
hiyo, ili kuthibitisha kama muda wake wa matumizi bado haujapita.
Makonda alisema, kuna taarifa kwamba wafanya biashara za vileo katika
Uwanja wa Fisi wamekuwa wakiuza viwaji hadi vilivyokwisha mda wake wa
matumizi.
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni Salum Hapi, akimpatia maelezo Makonda baada ya
kufika eneo la Uwanja wa Fisi, Tandale, kata ya Manzese.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wateja wa pombe
za kienyeji kwenye kilabu cha pombe hizo kilichopo Uwanja wa Fisi,
apofanya ziara katika eneo hilo leo
Mteja
wa pombe za kienyeji anayejiita Mandela, akikata kiu mbele ya Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na kutojua kuwa alikuwa
amekaa na Kiongozi
Kijana huyu ni miongoni mwa vijana wanaodaiwa kuwa wateja ambao hukesha Uwanja wa Fisi, naye alikuwepo leo
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiondoka kwenye eneo la Uwanja
wa Fisi baada ya kujionea mambo mbalimbali katika eneo hilo.
PICHA ZOTE
NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment