Mkurugenzi Mkuu wa Shieika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya kushirikiana kukuza sekta ya utalii nchini.
NA Mwandishi Wetu, Dar
BODI
ya Utalii nchini (TTB) na Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) limeingia
mkataba wa pamoja leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni lengo la kukuza soko
la Utalii wa ndani na kuongeza pato la taifa nchini.
Akizungumza
baada ya makabidhiano ya mkataba huo baina ya mkurugenzi wa
TTB DevotAha Mdachi na Mkurugenzi wa TTB Laislaus Matindi, Mwenyekiti
wa TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa uwepo wa shirika la
ndege la ATCL litasaidia katika ukuaji wa sekta ya utalii nchini kwani
italeta chachu kwa watalii wa ndani na wa nje kuja kwenda kwa wingi.
"Kwa
juhudi zilizofanywa na Rais John Magufuli za kurejesha uhai kwa kampuni
ya ATCL na kupata ndege zake ambazo zitasaidia kwenye kuutangaza utalii
kwa watalii wa ndani na nje kwani itasaidia pia kuinua na kukuza pato
;la taifa kwa kuingiza fedha za kugeni,"amesema Mihayo.
Mkataba
huo utakaowawezesha TTB kujitangaza Zaidi utawawezesha abiria
watakaokuwa wanasafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini kupata vipeperushi
vilivyozinduliwa leo vinavyoelezea baadhi ya vivutio vya utalii pamoja
na kuoneshwa kwa vituo hivyo kupitia TV za kwen ye ndege kuvionyesha.
Mwenyekiti
wa Shirika la ndege la ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso amesema kuwa kwa
safari za ndani katika mikoa mbalimbali, pia kwa sasa ATCL inataka
kuongeza safari za ndege kwenda katika mikoa mingine.
Kuongezeka
kwa safari hizo, pia kutachangia kwa watalii kutumia ndege za serikali
na kusaidia kuinua uchumi wa nchi na utakuwa ni endelevu ili kuimarisha
ushirikiano hiuo.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akikabidhiana mkataba na
Mkurugenzi wa ATCL Laislaus Matindi wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa TTB
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la ndege la
ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso leo Jijini Dar es salaam. Chini wakiwa
wanaweka saini ya makubaliano ya mkataba huo wakishuhidwa na mawakili wa
pande zote mbili.
Mwenyekiti
wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Kulia)pamoja na Mwenyekiti wa
Shirika la ndege la ATCL, Mhandisi Emmanuel Korroso wakionesha vijarada
vya Utalii vilivyozinduliwa leo Jijini Dar es salaam vitakavyokuwa
vinapatikana katika ndege za Shirika la ATCL.
wakurugenzi kutoka shirika la ndege la ATCL na bodi ya Utalii TTB wakiwa wanafuatilia kwa makini mkutano huo.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Shirika la Ndege la ATCL na Bodi ya Utalii TTB baada ya kumalizika kwa utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.
betmatik
ReplyDeletekralbet
betpark
tipobet
slot siteleri
kibris bahis siteleri
poker siteleri
bonus veren siteler
mobil ödeme bahis
YCMDL