DIWANI WA KILUNGULE, MBAGALA SAID FELLA AZINDUA UJENZI WA UZIO WA ZAHANATI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, July 17, 2016

DIWANI WA KILUNGULE, MBAGALA SAID FELLA AZINDUA UJENZI WA UZIO WA ZAHANATI

Diwani wa Kata ya Kilungule iliyopo Mbagala wilayani Temeke, Said Fella,akichimba msingi wa ukuta wakati wa ufunguzi wa ujenzi wa uzio wa zahanati ya kata ya kilungule,jijini Dar es Salaam, jana. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule, Barnabas Kayuni.

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wa Kata ya Kilungule iliyopo Mbagala wameshauriwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya kijamii ili kuondokana na kero ambazo zinawezekana kuzitatua wakishirikiana na viongozi wao na kuacha tabia ya kusubiria na kutegemea msaada kutoka serikalini.

Hayo yamesemwa na Diwani wa kata hiyo,Said Fella,wakati wa ufunguzi wa kujenga uzio wa eneo la itakapojengwa zahanati ya Kilungule iliyopo katika Mtaa wa Kilungule,Mbagala,jijini hapa jana ambapo alisema ombi la kujengwa zahanati katika kata ya Kilungule imekuja kufuatia usumbufu na umbali wa kilometa kumi ambazo wananchi wanakumbana nazo wakati wakihitaji huduma ya afya ambayo huelekea katika hospitali ya Zakhiem iliyopo Mbagala Rangi tatu na kusema amechangia matofali 1000 kwa ajili ya uzio huo ambapo halmashauri ya manispaa ya Temeke imekubali kuweka jengo lake katika eneo hilo.

Ameongeza kwa kusema kuwa wameamua kutengeneza uzio wa zahanati hiyo kwa nguvu za wananchi wa kata hiyo kabla ya ujenzi wake ambapo katika jengo hilo kutakuwa na sehemu ya kujifungulia kwa akinamama,matibabu madogo madogo na sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa kata ya kilungule na kata jirani na kupunguza matumizi ya fedha kuhudumiwa na kuhifadhi miili ya watu katika hospitali ya Zakhiem ambako kuna umbali mrefu wa kilometa 10.

“Kupatikana kwa Zahanati katika kata yetu itatupunguzia matumizi ya fedha kwenda kuhudumiwa katika hospitali ya Zakhiem pale Mbagala Rangi Tatu lakini pia itawasaidia akinamama kuondoa hofu ya kupoteza maisha kutokana na uzazi wakati wa kujifungua,matibabu kwa wananchi wote maana sisi sote ni wagonjwa watarajiwa pamoja na sehemu ya kuhifadhia miili yetu endapo hata mimi Said Fella mungu akinichukua nitahifadhiwa hapa hivyo nawaomba wanakilungule wote tujitoe kuhakikisha zahanati hii inapatikana” Alisema Fella

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule,Barnabas Kayuni,alisema kuwa wao kama serikali watatumia akili zao kuwashawishi wananchi kujumuika na kuchangia maendeleo katika mtaa wao ili kutatua kero za kijamii ikiwemo hilo la ujenzi wa uzio wa zahanati ya Kilingule.
Pia Mwenyekiti wa Nzasa A,Mzee Shefa,alisema katika mitaa mitano ya kata ya kilungule walikubaliana wachangie ili kumsapoti diwani wao kwa kuwa na kutoa mfano unapoenda kuomba mboga kwa mwenzako lazima uwe na mboga yako iliyochacha.  

Akizungumza kwa niaba ya akinamama wa kata hiyo,Uyaone Msonogole,alisema wanawake wengi wanapata tabu wakati wa kujifungua wengine wanajifungulia njiani wakipelekwa hospitali ya Zakhiem iliyopo Mbagala ambapo ni kilometa 10 kutokana kutokuwepo kwa zahanati katika mtaa,pia umbali huo umekuwa ukiwapotezea muda ambao wangeutumia katika kujiongezea kipato na kujiinua kiuchumi.

Hadi kumalizika kwa ujenzi wa uzio wa zahanati hiyo yanahitajika matofali 6700 yenye thamani ya Sh.Milioni 7 ukijumlisha simenti na vifaa vingine jumla yake ni milioni 70,wadau waliochangia ujenzi huo ni Tawi la Kilungule CCM wamechangia matofali 200,marafiki wa kata hiyo Sh.707,000,Kikundi cha Akinamama “Amani Federation” matofali 100,Mzee Muhenga matofali 200 wananchi wote wameombwa kujitolea kuchangia ujenzi wa uzio huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here