ZIMAMOTO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 29, 2016

ZIMAMOTO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

zim1
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
zim2
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Idd Chanyika (kulia) akitoa maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa Utawala naFedha, Billy Mwakatage walipotembelea banda hilo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
zim3
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuandikia mmoja ya mwananchi namba ya dharura 114 ambayo hutumika kupokea taarifa ya majanga mbalimbali kutoka kwa jamii.
zim4
Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam.
zim5
Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lililotumika kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto na maokozi lililopo katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Godfrey Peter, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here