Katibu
wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO
SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi
ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE
ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo
yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili
CHAMA
CHA ACT WAZALENDO
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Awali
ya yote, tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa kuitikia wito wa
kuja kutusikiliza. Karibuni sana!
Ndugu Waandishi wa Habari
Leo
tumewaiteni ili kuwaeleza msimamo wa Chama chetu cha ACT Wazalendo juu ya uamuzi
uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasimamisha
wabunge saba wa upinzani akiwemo Mbunge wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe.
Ikumbukwe
kuwa uamuzi huu wa Kamati ya Maadili ambayo sehemu kubwa ya wajumbe wake ni
wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) unafuatia msimamo wa wabunge wa upinzani
wakiongozwa na Mbunge wa Chama chetu kupigania maslahi ya wananchi kupata
habari za bunge.
ACT
tunaamini Wabunge hawa wametolewa kafara
kwa kupinga vikali uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja
kwa moja.
Ndugu waandishi wa Habari
Chama
chetu kimeandaa mapokezi haya yaliyopewa jina maalum la “Opereshen” Linda Demokrasia,
lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashujaa
hawa waliofukuzwa bungeni kwa ajili ya kusimamia maslahi ya umma,
kuelezea kilichotokea na kinachoendelea
bungeni ambacho watawala hawataki kijulikane.
Pia
katika mkutano wa hadhara Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Kabwe atafafanua kwa kina muktadha wa
siasa za sasa na hatari ya kuua vita dhidi ya ufisadi kutokana na namna
demokrasia inavyofifishwa.
Ndugu waandishi wa Habari
Kwa
kutambua umuhimu wa utetezi wa maslahi ya wananchi na kuisimamia serikali
kupitia Bunge Chama chetu baada ya mkutano wa Dar esSalaam utakaofanyika
Jumapili ya Juni 5 mwaka huu katika viwanja vya Mbagala Zakiem, pia Chama
kitafanya mikutano mingine mikubwa ya hadhara katika mikoa ya Mwanza ( 11 Juni, 2016), Kigoma (12 Juni,
2016), Mbeya (18 Juni, 2016) na Morogoro (19 Juni, 2016).
Chama
chetu kimeviandikia barua vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi kuviomba
kushiriki kwenye mapokezi hayo.Tunasubiri
majibu ya vyama tulivyowaalika kwa kuwaandikia barua kwa kuwa mpaka sasa
hawajatujibu rasmi kama watashiriki ama la zaidi ya kutufahamisha kuwa
wamepokea barua zetu
Ndugu Waandishi wa Habari
Sisi
ACT-Wazalendo,tunaamini “Operesheni Linda Demokrasia” ni muhimu ikapiganwa na
vyama vyote pasipo kujali itakadi ya vyama kwa kuwa hoja hiyo ya kutaka Bunge lioneshwe moja kwa
moja ilipoibuliwa na Mbunge Ndugu Zitto Kabwe
kuhoji hatua ya serikali kubana uwazi Bungeni,wabunge wote wa upinzani
walisimama na kuiunga mkono hoja na kuitetea.
Ndugu Waandishi wa Habari
Tunawashukuru
tena kwa kuitikia kwenu wito wa kufika na tunawatakia majukumu mema ya ujenzi
wa Taifa.
Ahsanteni
sana!
Ndugu
Ado Shaibu Ado
Katibu,
Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma,
ACT
Wazalendo
|
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Friday, June 3, 2016
Home
Unlabelled
ACT WATAJA RASMI SIKU YA KUMPOKEA ZITTO KABWE NA WABUNGE WA UKAWA, MIKUTANO ITAKAYOFANYIKA NCHI NZIMA
ACT WATAJA RASMI SIKU YA KUMPOKEA ZITTO KABWE NA WABUNGE WA UKAWA, MIKUTANO ITAKAYOFANYIKA NCHI NZIMA
About Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment