Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk. Thea Ntara akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi katika operesheni ya kukagua usafi wa mazingira ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu |
Afisa Afya Wilaya ya Kyela, Geophrey Baroshi akionesha aina ya pombe zilizopigwa marufuku kutumiwa na watu hapa nchini ambazo zilikutwa katika maduka zikiuzwa wilayani Kyela. |
Mkuu wa Wilaya akisimamiazoezi la kukagua aina ya vinywaji vilivyopigwa marufuku kutumiwa nchini |
Baadhi ya Wananchi wakishiriki katika usafi wa mazingira |
Baadhi ya vialabu vya pombe za kienyeji vikivunjwa kutokana na kutokudhi vigezo ikiwemo ukosefu wa vyoo |
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imeweka utaratibu kwa wananchi wake
kuhakikisha wanaepukana na magonjwa ya kuambukiza hususani kipindupindu
kwa kuwataka kila kaya kujenga vyoo.
Kutokana
na agizo hilo Watu 17 wakazi wa Kijiji cha Lusungo Kata ya
Lusungo wamekamatwa kwa kutokuwa na vyoo na uchafu wa mazingira
uliosababisha kuzorotesha juhudi za kupambana na ugonjwa wa
kipindupindu Wilayani humo.
Juhudi
hizo zimekuja baada ya ugonjwa huo kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu
ambapo Kata ya Lusungo na Ndobo ndizo pekee ambazo bado zina wagonjwa
wa kipindupindu hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk. Thea Ntara
kupiga kambi Kata ya Lusungo ili kufanya ukaguzi wa vyoo na usafi wa
mazingira.
Akizungumza
na gazeti hili katika ukaguzi huo, Mkuu wa Wilaya, Dk. Ntara alisema
anakwamishwa na Diwani wa Kata ya Lusungo Veronica Kanyanyila na
Mwenyekiti wa Kijiji Zawadi Lugano Mwangojola ambao wamekuwa wakidai
ugonjwa huo umesababishwa na imani za kishirikina na si uchafu au
ukosefu wa vyoo.
Katika
oparesheni hiyo maalumu iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya aliyeambatana na
Maafisa wa Afya pia iliyakumba maeneo mbalimbali kama Kata ya Ikama na
Kijiji cha Tenende ambapo alilazimika kuvunja Kilabu cha pombe Kata ya
Ikama baada ya kuwakuta wakazi wa eneo hilo wakinywa pombe za kienyeji
katika mazingira machafu.
Mbali
ya ukaguzi huo pia Mkuu wa Wilaya alishuhudia baadhi ya wananchi
wakinywa pombe ya moshi na pombe zilizopigwa marufuku kutoka nchi jirani
na kulazimika kuwakamata wahusika ambao wamefikishwa kituo kikuu cha
Polisi Wilaya ya Kyela ambapo pindi uchunguzi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani.
Pia
Mkuu huyo wa Wilaya aliteketeza sindano zinazodhaniwa kutumika kwa
ajili ya kujidunga na watumiaji wa madawa ya kulevya katika Kata ya
Ikama na ambapo alitoa agizo la kuwasaka wauzaji wa madawa hayo na
wanaouza pombe zilizopigwa marufuku kutoka nchi jirani.
Kwa
upande wake Afisa Afya Wilaya ya Kyela, Geophrey Baroshi alisema zoezi
hilo ni endelevu na watahakikisha kila kaya ina choo na kuwa na
mazingira safi kwa muda wote ili kuutokomeza kabisa ugonjwa huo Wilayani
Kyela na kwamba waliokamatwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Mtendaji
wa Kijiji cha Lusungo Fadhili Sade alisema wamefanya ukaguzi katika
kaya 681 za kijiji hicho na zote hazina vyoo hali inayofanya mapambano
ya kipindupindu kuwa magumu mno kwani wengi wao wamekuwa wakiamini
ugonjwa huo unatokana na ushirikina.
Naye
Mtendaji wa Kata ya Lusungo Stephen John alisema wamekuwa wakipokea
vitisho kutoka kwa Diwani wa Kata na Mwenyekiti wa kijiji kuwa aache
kutangaza kuwa Kata hiyo inakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu kwani
ndiyo kunachochea kuongezeka kwa ugonjwa huo ambao unatokana na ushikina
na si uchafu au ukosefu wa vyoo.
No comments:
Post a Comment