Dk Magufuli, juzi alikwenda
Mwanza kwa ziara maalumu ya kujitambulisha akitumia ndege ya Serikali aina ya
Fokker F28, jambo ambalo limeibua hisia tofauti.
Wakala
wa Ndege za Serikali (TGFA) imesema kuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) kilimlipia
Sh. milioni 8.4 mgombea urais wa chama hicho Dk. John Magufuli kwa ajili ya
kutumia ndege ya Serikali kwenda mkoani Mwanza kwenye ziara maalum ya
kujitambulisha.
Akizungumza
na Katuma Blog Ofisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, Kapteni
Keenan Mhaiki anasema chama hicho kilifuata taratibu zote zinazohusiana na
kukodi ndege hiyo na kusisitiza mtu au chama chochote kitakachohitaji huduma ya
usafiri hupatiwa kulingana na ratiba za viongozi wa serikali ambao
huitumia kwa safari mbalimbali.
“Hakuna
mtu aliyenyimwa ndege ukiona hajapatiwa kunatokana na ratiba yake kuwa
ngumu mara nyingine hutoa huduma ya usafiri timu za mipira zinaposafiri,”
alisema Kapteni Mhaiki.
Aidha,
anasema ndege hiyo hukodishwa bila upendeleo wa aina yoyote huku akisisitiza
hakuna mtu au chama kilichowahi kukodi kikanyimwa bali hutolewa kulingana na
nafasi iliyonayo.
Alisisitiza
kuwa TGFA itaendelea kufanya jitihada za kutoa elimu ya matumizi ya ndege
za serikali kwa jamii ili kuondoa dhana potofu iliyojengeka kuhusumatumiz
Julai
19, mwaka huu Dk. Magufuli alitumia ndege ya serikali aina ya Fokker F28 kwenda
Mwanza kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kugombea urais na Wajumbe
wa MKutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa( NEC)
uliofanyika Julai 12, 2015 mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment