MOSES MACHALI WA NCCR KUPOKELEWA ACT KESHO - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, July 20, 2015

MOSES MACHALI WA NCCR KUPOKELEWA ACT KESHO






 KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,kesho julai 21 atampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses  Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye atajiunga atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.


Machali ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna  wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini.,
 
Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini  yenye jumla ya kata 15 za uchaguzi
 
Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti wa matawi  101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648.wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini
 
Baada ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya jumamosi julai 25.
 
Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi.
 
Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama tofauti.

Abdallah Khamis
Afisa Habari -ACT-Wazalendo.
 Imetolewa leo julai 20/2015

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here