Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji akizungumza na waandishi Jijini Dar es Salaam |
SIKU
chache kupita baada ya Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa kukihama
chama chake cha awali cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema,navyo vyama vingine vya upinzania vimekishukia
Chadema na kusema kimeua upinzani nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jiijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Said Miraji wakati alipokuwa anazungumzia
suala la Lowassa kuhamia Chadema ambapo tayari ameshachukua fomu ya
Kugombani Urais kupitia Chadema. Chadema
ambao umeunda Vyama vya upinzani vya kutetea katiba ya Wananchi
UKAWA,ambapo Miradi amesema kwa sasa vyama vya upinzania vimejishusha
hadhi kwa watanzania.
“Kitendo hiki kimezidi kudhihirisha kuwa vyama vya upinzani
tunapozungumza vitu basi vinavyokuwa ni vya uongo,kwasababu Katibu mkuu
wa chadema Dakta Slaa aliaminisha umma kwamba lowassa ni miongoni mwa
mafisadi papa”
“Halafu
leo wamemkaribisha kwenye chama chao na kumpa nafasi ya Urais,sasa leo
watanzania watatuona sisi wapinzani ni waongo maana yale aliyoyasema
Slaa pale mwembe yanga ni uwongo au?”amehoji Miraji.
Miraji ameongeza kuwa kitendo cha chadema kumsimisha lowassa kunazidi
leta mpasuka kwa wananchama waliokijenga chama hicho kwa zaidi ya miaka
20.
“Inakuwaje mtu ahamie leo na leo hiyo apewe uongozi tena wa
juu,maana ndani ya chama hicho kuna makada waliokijenga chadema toka
1992 lakini leo hao hao hawapewi nafasi ya kugombani urais badala yake
leo unawatupa unampa mtu aliyekuja leo kisa anaumaarufu wa watu,je hivi
unategemea wananchi wengine hawatakubali”ameongeza.
Aidha Miraji amekitahadharisha Chadema kuacha tabia ya kutegemea
kuwachukua wabunge na madiwani kutoka CCM na kuwapa uongozi kwa kusema
suala hilo litaweza kukivuruga chama hicho kwa madai ya kuwa CCM
wamepandikiza watu wake kuja kumaliza upinzani nchini.
No comments:
Post a Comment