GWIJI wa Juventus na Real Madrid Zinedine Zidane amesema Paul
Pogba anapaswa kuhamia Hispania kama anataka kuondoka kwa mabingwa wa Italia.
Pogba amekuwa na msaada mkubwa kwa Juvemtus msimu huu hali
iliyoibua mjadala wa kutakiwa na timu mbalimbali miezi ya karibuni, na Real
ikiwa miongoni mwa timu zinazomuwania.
Na Zidane anayeifundisha timu ya Castilla ya Real alisema Pogba
atakuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na mabingwa hao mara 10 wa Ulaya.
"Sijui ataishia wapi, sina taraifa zake,” alisema mchezaji
huyo wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa alipozungumza na Radio Monte Carlo.
"Pogba anakiwango cha kucheza anavyotaka, na kwa sasa
kama anataka kuondoka Juventus namuomba aende Real Madrid na wachezaji wote
bora wanacheza hapa,hivyo nadhani itakuwa nzuri kwake kuja,”.
"Lakini kwa sasa hili si jambo muhimu sana, anamaamuzi
yake,”.
Pogba anatarajiwa kuonyesha makali yake kwenye fainali za Ligi
ya Mabingwa Ulaya leo ambapo timu yake itacheza na wapinzani wa Real ,Barcelona
mjini Berlin.
No comments:
Post a Comment