TABIA ya watu kukwepa kutoa ushahidi mahakamani,
imetajwa kuwa sababu mojawapo inayochangia kukosekana kwa ushahidi dhidi ya
wahalifu wa mauaji ya albino.
Hayo yalielezwa katika warsha zilizoendeshwa mfululizo
wilayani Misungwi, Kahama na Bariadi za ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia
na kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa
ngozi nchini.
Wakichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili watu
wenye ulemavu wa ngozi, washiriki wamesema imekuwa kawaida kwa watu kutokuwa
tayari kutoa ushahidi mara wanapoitwa mahakamani, kwa sababu zisizokuwa na
mashiko.
Sababu hizo ni kuogopa kuuawa na wahusika na shinikizo
kutoka kwa wanafamilia.
No comments:
Post a Comment