WIMBO wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira
wa ‘Mkuhumi’ umezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam, huku ukitarajiwa kuleta
mabadiliko miongoni mwa wananchi.
Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya
Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na mwanamuziki wa kughani
mashairi, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini
(Mjumita), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni
rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.
Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha
wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza
Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu
(Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda...
“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko
kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa
rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu
tutawafgikia watu wengi,” alisema.
Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi
wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze
kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko
ya tabia nchi.
“Kupitia wimbo huu jamii itapata uelewa
utakaosaidia kuhamasisha jamiikutumia rasilimali za misitu kwa njia ya
uendelevu na kujipatia faida,” alisema Njaidi.
No comments:
Post a Comment