LOWASSA
 |
| Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na Wanachama
wa CCM na wananchi katika Uwanja Samora Mjini Iringa baada ya
kukabidhiwa majina ya wanaCCM zaidi ya 58 elfu waliomdhamini kugombea
urais katika Mkoa huo |
ASKOFU wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dayosisi ya Iringa, Dk Owdenburg Mdegella ameungana na maelfu ya wakazi wa mkoa
wa Iringa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika harakati
zake za kutafuta ridhaa ya
CCM
ili awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Zaidi
ya wanaCCM 58,000 wakiwemo zaidi ya 23,000 wa Manispaa ya Iringa ambayo
mwaka
2010 ilipoteza jimbo la Iringa Mjini kwa Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema,
walitangazwa na Katibu Mwenezi wa CCM Manispaa ya Iringa, Thobias Kikulacho
kumdhamini mgombea huyo.
Mbali
na Askofu Mdegella viongozi wengine wa dini waliojitokeza kuiombea mema
Safari
ya matumaini ya Lowassa ni pamoja na Askofu Mkuu wa Makanisa ya End Time and
Harvesting, Dk Boaz Sollo na baadhi ya mashehe wa mjini Iringa......
Wingi
wa wadhamini hao pamoja na mamia ya wananchi waliojitokeza juzi kushuhudia
tukio la Lowassa kudhaminiwa ulisababisha shughuli hiyo kufanyikia Uwanja wa
Michezo wa Samora, badala ya ofisi CCM mkoa.
Akiiombea
mema safari ya Lowassa, Askofu Mdegella alisema “Hata kama wanaoamua nani awe
kiongozi ni wachache ni lazima wasikilize watu wanataka nani, mimi naamini
wanaCCM wote ni wasikivu kwa watu; Iringa na kwingineko watu wameongea si kwa
maneno ila kwa matendo.”
MEMBE
KATIKA hali inayoweza kuhitimishwa kama ukomavu wa
kisiasa, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amemmwagia sifa mwanasiasa mwenziwe
Makongoro Nyerere akimpambanua na sifa ya ujasiri wa kukemea maovu
bila
kuogopa.
Membe
amesema Tanzania inahitaji viongozi aina ya Makongoro Nyerere kukemea madhambi
ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi, CCM.
“Ninavutiwa
sana na ujasiri alionao mwanasiasa na mgombea mwenzangu Makongoro Nyerere kwa
kukemea ufisadi waziwazi bila hofu yoyote, ninaunga mkono ujasiri huo maana
hata mimi ninachukiwa sana na wapenda rushwa na ufisadi ndani na hata nje ya
chama chetu.”
Waziri
Membe aliyasema hayo juzi wakati akitoa shukrani kwa wanachama zaidi ya 1900 wa
chama hicho waliojitokeza kumdhamini kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara.
“Mkoa
wa Mara ni mkoa wenye heshima kubwa maana ni katika ardhi hii Mwalimu Julius
Nyerere alizaliwa akiwa ni mtu aliyechukia dhuluma, rushwa na ufisadi na
mwanawe, mgombea mwenzangu naye kachukua nyayo hizo, anakemea wazi wazi vitendo
vya rushwa,” alisema.
PROFESA MWANDOSYA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, Profesa
Mark Mwandosya amemuomba mgombea mwenzake katika kinyang’anyiro cha kutafuta
ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea kupitia CCM, Edward Lowassa asisite kumuunga
mkono kama walivyofanya watangaza nia wengine ili mambo yaishe mapema.
Aidha,
amewaonya wanaotishia kukihama chama endapo hawatapitishwa, akisema huo ni
upuuzi na pia vitisho kwa Mwenyekiti wa Chama na wanaCCM kwa ujumla, hivyo
wanaojiona wao ni maarufu kuliko chama wanajidanganya.
Mwandosya
alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wilayani Mbozi alipokuwa akizungumza na
wanaCCM waliomdhamini katika mbio zake za urais, pamoja na wanachama wengine
waliojitokeza katika Ofisi za CCM Wilaya.
Mgombea
huyo alisema amefarijika kusikia anaungwa mkono na wagombea wenzake,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe pamoja na kupata taarifa za Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Stephen Wassira naye kusema anamuunga mkono.
Alisema
pamoja na kuungwa mkono na wenzako hao watatu, anamuomba pia Lowassa naye
kumuunga mkono ili kuipunguzia kazi Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM).
“Nimesikia
Membe amesema hapa Mbeya asipopitishwa yeye basi atamuunga mkono Profesa
Mwandosya, nikasikia tena na Waziri Mkuu akisema hata kama asipopitishwa yeye
atafarijika kama Profesa Mwandosya atakuwa mgombea, nikasikia tena na Wassira
naye kupitia kwa mtu wake wa karibu ataniunga mkono, sasa namuomba mwenzangu
naye Edward au maarufu kama Edo naye aseme Profesa ndiyo wangu, ili kazi
iishe na tuipunguzie kazi Halmashauri Kuu,” alisema Profesa na kushangiliwa.
Awali
Profesa Mwandosya aliwaeleza wanachama hao kuwa mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka
mgumu sana kwa CCM na kuwataka wanachama kutofanya mchezo katika kujibu mapigo
ya wapinzani.
“Watatuuliza
kuhusu EPA, wataendelea kutuuliza kuhusu Richmond, watatuuliza kuhusu Escrow,
kubwa zaidi watatuuliza kuhusu Vodacom ingawa hili halizungumzwi lakini
linakuja, lazima tujitayarishe.
“Sasa
nani huyo ataweza kutusafisha, wananchi wakimtazama watasema huyu atatusaidia
na atajibu, kila ninakopita naambiwa na wananchi kuhusu ufisadi na rushwa
vinatuumiza. Kama chama lazima tukabiliane na hilo na hapa hatumzungumzii mtu
lazima kama chama tuyaeleze kwa wananchi. Nani atafanya hivyo wakubwa wanajua,”
alisema Profesa.
Akizungumzia
wanaotishia kuhama chama, alisema wanajidanganya kwani CCM ni maarufu zaidi ya
mtu mmoja mmoja, akisema mtu pekee aliyewahi kuhama na kukitikisa chama alikuwa
Augustine Mrema, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani.
DK MWAKYEMBE
WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison
Mwakyembe amesema kati ya mambo anayoweza kujivunia wakati wa utawala wa
serikali ya awamu ya nne ni kuwa miongoni mwa washauri wazuri wa Rais Jakaya
Kikwete.
Alisema
ni mmoja wa mawaziri wanaomshauri katika kusimamia na kutekeleza mambo ya
maendeleo ambayo yamewezesha kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
Aidha,
amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuna watu tena baadhi yao wako ndani
ya CCM wanajifanya hawajaona maendeleo ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa
barabara za lami zinazounganisha kati ya mkoa mmoja na mwingine, maji, afya,
elimu na mingineyo.
Alisema,
serikali ya awamu ya nne inapaswa kupongezwa kutokana na utendaji wake mzuri
katika kubuni, kutekeleza na kufuatilia miradi yote iliyopangwa na hiyo inampa
sifa kubwa yeye na kumfanya kuwa miongoni mwa watu wenye uwezo wa kugombea
Urais wa Tanzania kupitia CCM.
Aliyasema
hayo jana mjini Songea wakati akiwashukuru wanachama wa CCM waliomdhamini
katika harakati zake za kuomba ridhaa ya CCM ili awe mgombea wake, huku
akisisitiza kuwa anajiona ana sifa nyingi, ndiyo maana amejitokeza aweze
kuendeleza mema yaliyofanywa na Serikali ya Rais Kikwete.
No comments:
Post a Comment