WINGA wa Manchester United, Angel di Maria amesisitiza kwamba
atabaki Old Trafford msimu ujao.
Di Maria amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia kwa mabingwa wa
Ufaransa, Paris Saint-Germain au miamba ya Ujerumani Bayern Munich baada ya kuwa
na msimu mbaya wa Ligi Kuu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alishindwa kufanya
vizuri, licha ya kufanya uhamisho wa gharama wa pauni milioni 59.7.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid amejikuta akisugua
benchi kuanzia Machi mpaka mechi ya mwisho ya msimu.
Aidha, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hana mpango wa
kuondoka Old Trafford akijiandaa na
michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza Chile wiki ijayo.
"Ndio kwanza nimemaliza msimu wangu wa kwanza kuichezea
Manchester United," Di Maria alikaririwa kwenye the Sun.
"Ulikuwa msimu mgumu kwangu, nadhani ulikuwa mgumu kwa
sababu ilikuwa nchi nyingine na ligi nyingine na ligi hii ni ngumu kuliko ya
Hispania, hivyo sikuweza kumudu mwenyewe kama nilivyokuwa nikitaka.
"Sasa nitacheza kwenye Copa America na kisha nitarudi
Manchester kwa ajili ya msimu ujao na kufanya vizuri”.
Di Maria amesaidia mabao 10 na kufunga matatu katika mechi 27
za Ligi Kuu alizocheza msimu uliopita United ilipomaliza nafasi ya nne na
kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa
No comments:
Post a Comment